September 28, 2017



Baada ya Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, kukaa hivi karibuni imepitia taarifa mbalimbali ya michezo iliyofanyika ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza na kufikia uamuzi ufuatao.

Mechi namba 2 Kundi A (Mvuvumwa v African Lyon). Timu ya Mvuvumwa FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi ya mechi na kuhudhuria wakiwa pungufu. Pia timu hiyo ilichelewa kufika uwanjani ambapo ilifika saa 9.20 mchana badala ya saa 9.00 mchana.

Adhabu dhidi ya Mvuvumwa FC imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza. Kwa kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi ya mechi, uwanjani na kuhudhuria kikao wakiwa pungufu ni ukiukaji wa Kanuni za 14(2a) na 14(9) za Ligi Daraja la Kwanza.

Mechi namba 1 Kundi B (Mlale JKT v Polisi Tanzania).
 Timu JKT Mlale imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa kosa la kuchelewa kufika uwanjani. Iliingia saa 9:20 mchana badala ya saa 9:00 mchana. Kitendo hicho ni uvunjifu wa Kanuni ya 14(9) ya Ligi Daraja la Kwanza, na adhabu dhidi yao ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic