September 8, 2017

 
KLABU ya Yanga, jana ilifanikiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya Uhai Production Media Group, kwa ajili ya kurusha matangazo yake ya kipindi cha television ‘Yanga TV’ katika moja ya chaneli za Azam TV. 

Kwa kusaini mkataba huo kwa Yanga inakuwa inaungana na mahasimu zao wakuu, Simba ambao tayari muda mrefu walikuwa wameingia makubaliano na kampuni hiyo kwa ajili ya kurusha kipindi chake katika Simba TV. 

Akizungumza  Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, amekiri kusaini mkataba wa miaka mitatu na Azam TV ambapo sasa utaipatia fursa klabu hiyo ya kuongeza kipato kupitia Azam TV, tofauti na hapo mwanzo ambapo hawakuweza kufikia mwafaka. 

“Ni kweli tumesaini mkataba wa kurusha matangazo yetu Azam TV, japo siyo suala geni sana kwetu kwani huko mwanzo tuliwahi kufanya nao mazungumzo kabla hata ya Simba ambao wao waliingia nao makubaliano kipindi hicho. 

“Tumefanya hivi kwa maana nzuri ya kuiongezea kipato klabu yetu ambapo tumekubaliana kuwa mkataba huu utakuwa ukidumu ndani ya miaka mitatu mitatu na baadaye tutakuwa tukikaa mezani na kuupitia upya kulingana na mahitaji ya kipindi hicho yatakavyokuwa. 
“Huko nyuma hatukuweza kufanya hivyo kutokana na hali halisi ya uongozi wa juu kutoafikiana ila kwangu mimi ninalazimika kupanua wigo wa pato la klabu ili iweze kujiendesha yenyewe pasipo kuwa tegemezi. 

“Ndiyo maana utaona napambana na wenzangu kufungua vyanzo vingi vya mapato kwa lengo la kuifanya ikidhi baadhi ya mahitaji ambayo yamekuwa changamoto kwetu,” alisema Sanga ambaye anakaimu nafasi ya uenyekiti iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa mwenyekiti, Yusuf Manji kujiuzulu.

5 COMMENTS:

  1. Namuelewa Sanga kwenye hili. Naamini bado hatujachelewa angalau tunatakiwa kuongeza spidi zaidi.
    Naona nguvu ya uwekezaji kupitia wadhamin inatakiwa kuongezeka zaidi. Tunao Vodacom kifuani..tujaribu na hizi Financial Institutions au kampuni za vinywaji,madini na wadhamini wengine.
    Kwa mfano tujaribu kuongea Na voda ili vifaa vya mazoez na tutakavyotumia muda wa kuweka misuli sawa tutumie vya wadhamin wengne

    ReplyDelete
  2. Ni muda wa kutafuta ubia wa kujenga uwanja. Yanga ni taasisi kubwa ukiondoka Sanga mwengne ataendelea si kwamba deni litakuwa LA kwako.
    Tuongee Na NSSF or LAPF Na hata mashirika mengne yajenge uwanja alafu watukate kwa kila mechi tutakayocheza.
    Najua itawezekana kwa hlo. Tuoneshe mfano ili tupige hatua. Tusibaki Na fikra mgando tutanue mawazo yetu. Shirikiana Na wanachma Na wapenz. Kuna kitu kitakuja kuwa chenye manufaw

    ReplyDelete
  3. Tunahitaji mipango Kama hiyo iongezeke zaidi kutafuta mapato ya timu. Kama walivyotangulia kusema wenzangu Kwenye comments za awali kuwa Yanga ni timu kubwa itafute wadhamini zaidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic