October 21, 2017



Wanachama na mashabiki wa Yanga hasa wale maarufu kama Makomandoo wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na mashabiki wa Stand United na kushambuliwa.

Baadaye, polisi walilazimika kuingia uwanjani hapo kutuliza hali ya hewa ambayo ilikuwa imechafuka.

Yanga iko mjini Shinyanga na kesho itawavaa Stand United katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage.


Mashabiki hao wa Stand wameanzisha tafrani kubwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga baada ya mzozo kati yao kuzuka leo asubuhi.

Awali hakukuwa na tatizo, lakini tafrani lilianza baada ya Yanga kufika kwenye Uwanja wa Kambarage wakitaka kufanya zoezi lakini Stand nao waliwasili pale na kusema wao ndiyo wenyeji na Yanga kama wageni walitakiwa kufanya mazoezi jioni.

Baada ya hapo, Yanga walikubali na kuwaambia Stand wakimaliza, wao Yanga wataendelea. Wakakubalia.

Shida ilianza pale baada ya Stand kumaliza na kuondika, Yanga wakaanza kujiandaa kufanya mazoezi na wale wanachama wa Yanga na mashabiki wao wakawataka wale wa Stand kuondoka uwanjani hapo.

Hali hiyo ilianzisha fujo kwa kwua mashabiki hao wa Stand nao walihoji kuwa Yanga bao waliangalia mazoezi ya timu yao na hawakutoka nje.

Pia waliendelea kusisitiza kuwa ni uwanja wao hakuna anayeweza kuwafukuza na hapo ugomvi ulianza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic