October 31, 2017




Msimamo wa Ligi Kuu Bara unaifanya ligi hiyo kuwa ngumu zaidi katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 katika mechi 8 za mwanzo.

Baada ya kila timu kucheza mechi 8, inaonyesha timu nne za juu zimeendelea kufunga kwa pointi.

Jambo hili ni aghalabu kutokea katika Ligi Kuu Bara na mara nyingi, Yanga, Simba na Azam FC katika miaka minne iliyopita zimekuwa zikifukuzana kileleni lakini angalau kwa tofauti ya pointi mbili hadi nne au tano.

Lakini safari hii, Simba walio kileleni wana pointi 16 sawa na nafasi ya pili waliyo Yanga pia Mtibwa Sugar na Azam FC katika nafasi ya tatu na nne.

Ulingano huo umeanzia katika mechi ya sita na mambo yameendelea hivyo hadi sasa timu hizo zikiendelea kufungana pointi.

Hata hivyo, inaonyesha kuna nafasi kubwa ya mambo kubadilika kama kuna timu moja itapoteza na huenda mvurugano ukaanza wikiendi ijayo.

Timu zilizo nafasi ya tano na sita, yaani Singida United na Prisons nazo zimefungana pointi zikiwa na 13 kila moja na zinaonyesha kuwa na nafasi ya kufikisha 16 na kuzifikia nne za juu kama moja wapo itateleza na hizi mbili kushinda.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic