October 31, 2017


Simba wameamua kurejea kazini kuhakikisha mambo yanaendelea ikiwa ni baada ya gumzo la sare dhidik ya Yanga.

Kiongozi mmoja wa Simba ameiambia SALEHJEMBE kwamba sare dhidi ya Yanga imeonekana kuwavuruga kwa kuwa hakuna iliyemfurahisha.

“Simba mnaweza mkafungwa lakini angalau mcheze mpira, lakini kama wapinzani ndiyo wanacheza mpira na nyie hamjashinda, basi ujue kuna tatizo.

“Lakini kinachotakiwa maisha yaendelee, hakuna cha kusema kuwa tumesikitika halafu tuendelee kusikitika. Ligi bado inaendelea na lazima tupambane,” alisema.

Simba imeendelea na mazoezi kujifua kwa ajili ya mechi zijazo kwa kuwa iko kileleni kwa tofauti ya mabao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic