Baada ya kucheza mechi dhidi ya Njombe Mji kikosi cha Simba kinatarajia kumchezesha Mchezaji Mohammed Ibrahim Mo kwenye mechi dhidi ya Yanga, Jumamosi ijayo.
Mo alicheza mechi iliyopita ya Simba dhidi ya Njombe Mji na kufanikiwa kuonyesha kiwango kizuri.
Msemaji wa Simba Haji Manara alisema mchezaji huyo kwa sasa yupo fiti na anaweza kucheza mechi yoyote ijayo kama kocha akiamua kumtumia.
Simba imeweka kambi Unguja visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo ya Jumamosi, na kiungo huyo ameonekana kupambana sana kuhakikisha anacheza.
“Mo yupo vizuri na anaendelea na mazoezi na wenzake, ni jambo la kocha tu kuamua, lakini anaweza kucheza michezo ijayo ukiwemo dhidi ya Yanga.
“Kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji alicheza vizuri na kocha alivutiwa na kiwango chake,” alisema Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment