October 28, 2017



Kocha wa Yanga, Geoge Lwandamina, leo analazimika kumrejesha kiungo wake, Papy Kabamba Tshishimbi kucheza nafasi yake ya kiungo mkabaji badala ya kiungo mshambuliaji aliyocheza mechi iliyopita.

Katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Stand United, Tshishimbi alichezeshwa nafasi ya kiungo mshambuliaji huku Pato Ngonyani akicheza nafasi ya kiungo mkabaji.

Lwandamina akiwa kambini Morogoro ameamua kumrejesha Tshishimbi katika nafasi ya kiungo mkabaji ili aweze kutibua mipango ya washambuliaji wa Simba akiwemo Emmanuel Okwi.

Yanga ilirejea Dar es Salaam, jana saa 3:00 asubuhi kwa usiri mkubwa na kujichimbia jijini ambako jioni walitarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi ya leo.

Ndani ya benchi la ufundi, taarifa zinaeleza kuwa Tshishimbi amerejeshwa kucheza kiungo namba sita ili
kupunguza makali ya washambuliaji wa Simba ambao ni Okwi, Laudit Mavugo na Shiza Kichuya.

Alisema kwa mabadiliko hayo, Tshishimbi atacheza namba sita halafu Raphael Daud atacheza namba nane kwani hakuna uhakika wa Thabani Kamusoko kucheza kutoakana na kuwa majeruhi.

“Katika mechi hii dhidi ya Simba kikosi chetu kinatarajiwa kuwa na mabadiliko kidogo kinachotarajiwa kuwa tofauti na mechi iliyopita na Stand United.

“Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuwa kama ifuatavyo, Tshishimbi hatacheza namba nane kama alivyocheza awali na badala yake atacheza namba sita ambayo mchezo uliopita alicheza Pato Ngonyani.

“Upo uwezekano mkubwa wa Raphael akaanza kucheza namba nane akisaidiana na Paul Buswita katika safu ya kiungo kutokana na maandalizi aliyoyafanya kocha, kwani Kamusoko ni majeruhi,” alisema mtoa taarifa huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic