November 10, 2017




Kesi ya utakakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mwesigwa Selestine, jana iliahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mpaka Novemba 17, mwaka huu.

Mbali na Malinzi na Mwesigwa kurudishwa rumande katika Gereza la Keko, pia aliyekuwa Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ nao walipandishwa katika mahakama hiyo na kurudishwa rumande mpaka Novemba 17, mwaka huu.

Malinzi na Mwesigwa, walipandishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri ambapo kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika, wakarudishwa rumande.

Awali upande wa utetezi wa watuhumiwa hao, uliwasilisha ombi kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kuwepo mahakamani hapo ili kutoa maelezo ya upelelezi huo ulipofikia, lakini ombi lao lilitupiliwa mbali kutokana na kile kilichoelezwa kwamba, wakili wa serikali anavyofanya kazi ni sawa na DPP.

Kwa upande wa Aveva na Kaburu wanaotuhumiwa kutakatisha fedha, wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, alisema upelelezi bado haujakamilika, hivyo kesi hiyo haiwezi kusikilizwa kwa sasa.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa ambaye ndiye anasikiliza kesi hiyo, aliutaka upande wa mashitaka kufanya haraka katika upelelezi wao ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.
  


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic