November 10, 2017



Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu ameonekana kumpa moyo kiungo na nahodha wa zamani wa Simba, Jonas Mkude.

Ajibu amemuambia Mkude kuwa iko siku thamani yake itajulikana huku akimsifia kuwa kiungo bora kabisa.

Straika huyo wa Yanga amefanya hivyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram.

"Maestro midfield, ipo siku thamani yako itaonekana kaka," anaandika Ajibu.

Mkude amekuwa akiendelea kubaki benchi kwa muda wakati Kocha Joseph Omog amekuwa akimuamini zaidi James Kotei, raia wa Ghana.

Lakini katika mechi mbili zilizopita, inaonekana Omog ameanza kumuamini zaidi Mkude.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic