Wataalamu wa masuala ya usajili katika soka barani Ulaya wanaonekana kushangazwa na FC Barcelona kuendelea kuwa kimya na kutosaini mkataba na Lionel Messi, hadi sasa.
Mkataba kati ya Messi na Barcelona utaisha Juni, 2018. Maana yake, ifikapo Januari Mosi, mwakani, atakuwa huru.
Uhuru utamfanya Messi awe tayari kuzungumza na klabu yoyote na hii itakuwa na ugumu mkubwa kwa Barcelona kuhakikisha wanambakiza bila kuingia gharama kubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment