November 4, 2017



Mbeya City hawajataka hata kupoteza muda kwa kukata kona baada ya kusema kuwa hata kidogo 
hawatishwi na washambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi, Emmanuel Okwi na Laudit Mavugo.

Mechi ya Mbeya City na Simba ambayo ni namba 72 katika Ligi Kuu Bara msimu huu, itachezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na tayari Simba imeshaingia Mbeya tangu jana.

Kocha wa Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo amesema amejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda dhidi ya Simba bila ya kuwahofia nyota wake Okwi raia wa Uganda na Mavugo raia wa Burundi.

“Maandalizi ya kucheza na Simba yanaendelea vizuri, Simba ni timu kubwa lakini kwetu haitokuwa mechi nyepesi kwa sababu tumewaona katika mchezo uliopita wakicheza na Yanga.

“Tunataka ushindi na hatuwezi kuhofia mchezaji wao mmoja mmoja, hatuna cha kuogopa, wachezaji wao wote ni wa kawaida na wapo kwenye kiwango kimoja,” alisema Nsanzurwimo.

Nsanzurwimo, raia wa Burundi, alijiunga na Mbeya City hivi karibuni kuchukua nafasi ya Kinnah Phiri aliyetimuliwa lakini amefanikiwa kukaa benchi kwenye mechi mbili.


Katika mechi hizo, alitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mbao FC halafu akafungwa bao 1-0 na Azam FC wiki iliyopita. Sasa anakutana na Simba ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 16 wakati Mbeya City ni ya nane ikiwa na pointi 11.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic