November 16, 2017



Hatimaye, uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umekanusha juu ya taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa zikiwahusu vigogo wa shirikisho hilo wakiongozwa na rais wao, Wallace Karia kujilipa posho ya kiwango cha juu.

Hivi karibuni kulisambaa taarifa mitandaoni juu ya vigogo hao wa TFF kujilipa fedha nyingi. 

Kumbuka viongozi wa kuchaguliwa TFF hawapati mishahara, badala yake wanalipwa posho, sasa ilielezwa kwamba Karia analipwa Sh milioni sita, makamu wake Sh milioni tano huku wajumbe wa Kamati ya Utendaji wakilipwa milioni moja kwa kila mwezi.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amesema suala hilo halina ukweli na kudai kuwa Karia alikataa kulipwa na kusisitiza posho yake ipelekwe katika masuala mingine ya kimpira kwa kuwa yeye ni muajiriwa wa serikalini na analipwa mshahara huko.

“Hizo taarifa hazina ukweli wowote kwa sababu viongozi wa hapa hakuna ambaye anachukua kiasi hicho cha fedha.


“Hata kwenye suala la wajumbe, nao hakuna ambaye anapokea shilingi milioni moja kwa mwezi kama inavyosemekana badala yake tunatoa shilingi milioni moja na nusu kwa miezi mitatu tena kwa yule ambaye anachakarika na tunaona juhudi zake kwa kupitia ripoti ambazo anawasilisha kwenye vikao.


“Lakini kwa sababu jambo hilo limechafua sura ya taasisi yetu tuna mpango wa kuwafungulia kesi ya makosa ya kimtandao wale wote ambao wamehusika kwenye suala hilo na tayari tuna majina 10 ya watu ambao tutaanza nao,” alisema Kidau.

Pamoja na TFF kuamua kulitolea ufafanuzi suala hilo, bado inaonekana haukuwa mjadala mpana hasa nje ya mitandao na huenda waliamua kuwahi mapema ili kumaliza mjadala.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic