November 5, 2017


Deontay Wilder amemtwanga  Bermane Stiverne katika pambano lao la uzito wa juu na baada ya kutangazwa mshindi, akasema waziwazi kwamba sasa anamtaka Anthony Joshua. 

Wilder ameshinda katika raundi ya kwanza tu baada ya kumvurumishia mpinzani wake makonde utadhani mvua za masika.


Sasa anachotaka ni kumvaa Joshua raia wa Uingereza ili kumaliza ubishi.

Ubishi mkubwa upo kati ya Mmarekani huyo na Muingereza huyo nani ni mkali zaidi.


Lakini kipigo kikali alichotoa Wilder kwa Stiverne kinafanya wengi waaamini atakuwa maji marefu kwa Joshua lakini wako wanaosisitiza Joshua ni Joshua lakini lazima aimarishe kiwango chake kwanza.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic