December 11, 2017


Arsenal imepangwa kucheza dhidi ya timu ya Ostersunds ya nchini Sweden katika Hatua ya 32 Bora ya michuano ya Europa League.

Arsenal itawavaa wapinzani wao hao ambao wanafundishwa na Graham Potter ambaye ni raia wa Uingereza.

Atletico Madrid wao wamepangwa kukutana na Copenhagen wakati Borussia Dortmund itakutana na wabishi kutoka Italia, Atalanta ambao waliifunga Everton nyumbani na ugenini katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Makocha wawili waliowahi kufanya kazi England wanatarajia kukutana pia katika hatua hiyo wakati ambapo Celtic inayonolewa na Brendan Rodgers itakutana na Zenit St Petersburg iliyochini ya Roberto Mancini.

Kocha Gennaro Gattuso wa AC Milan ataiongoza timu yake hiyo kuivaaa Ludugorets ya Bulgaria.

Ratiba kamili inaonyesha hatua hiyo itachezwa Februari 15 wakati mechi za marudio ni Februari 22, mwakani 2018. 

RATIBA KAMILI YA 32 
Borussia Dortmund vs Atalanta

Nice vs Lokomotiv Moscow

Copenhagen vs Atletico Madrid

Spartak Moscow vs Athletic Bilbao

AEK Athens vs Dynamo Kiev

Celtic vs Zenit St Petersburg

Napoli vs Leipzig

Red Star Belgrade vs CSKA Moscow

Lyon vs Villarreal

Real Sociedad vs Salzbug

Partizan Belgrade vs Viktoria Plzen

Steaua Bucharest vs Lazio

Ludogorets vs AC Milan

Astana vs Sporting Lisbon

Ostersunds vs Arsenal

Marseille vs Braga 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV