December 6, 2017



Mwanamichezo, Joel Nkaya Bendera amefariki dunia.



Bendera ambaye ni mwanasiasa mkongwe na aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania iliyoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 1980, amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, leo saa 10 na dakika 24 jioni.

Alipokelewa Muhimbili Saa 6 mchana akitokea katika hospitali ya Bagamoyo ambako alilazimwa mwanzo.

Kabla alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), hospitalini hapo na taarifa za kuwa alifariki dunia zilisambaa mtandaoni na mkewe akazikanusha.

Lakini baadaye ilitoka taarifa rasmi kuwa Bendera aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro na baadaye Manyara alifariki dunia.

Bendera aliwahi kuwa mbunge na waziri lakini aliwahi kuwa mwalimu wa chuo cha michezo Malya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic