December 15, 2017


Kocha Hemed Morocco amesema ana imani kikosi chake cha Zanzibar Heroes kitafanya vizuri dhidi ya Uganda katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Chalenji, leo.

Hata hivyo, kocha huyo amelaani kitendo cha Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kuwapima wachezaji wa Zanzibar kama wanatumia dawa za kusisimua misuri.

Morocco amesema suala hilo halikuwa sawa kwa kuwa kuihofia Zanzibar pekee kwa kuwa imeonyesha kupanda kisoka, si jambo zuri.

“Angalau na wengine wangepimwa ili tujue, tena wapimwe na itangazwe hivi katika vyombo vya habari.

“Naona haikuwa sahihi, soka la Zanzibar linakwenda linapanda na niwambie, hakuna mchezaji wa Zanzibar anaweza kutumia dawa hizo ambazo kwanza ni kama shilingi laki tatu za Kitanzania,” alisema.

Kuhusiana na mechi alisisitiza, Uganda ambao ni mabingwa watetezi ni timu ngumu lakini watapambana hadi mwisho kwa kuwa wamenuia kufika fainali na ikiwezekana kubeba kombe.


Kikosi cha Zanzibar Heroes, kimeendelea kuonyesha soka safi katika michuano hiyo na sasa ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania walio katika michuano hiyo baada ya Kilimanjaro Stars kutoka Bara kuwa mdebwedo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic