December 1, 2017




Straika wa KRC Genk, Mbwana Samatta, ameanza kuonyesha matumaini kwa klabu yake kutokana na maendeleo yake kuwa mazuri na huenda akarejea uwanjani mwishoni mwa mwezi huu.

Samatta aliumia goti Novemba mwanzoni katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji  kati ya K.R.C Genk dhidi ya Lokeren ambao ulimalizika kwa 0-0, baada ya vipimo ilionekana atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita au zaidi.

Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo, amesema kuwa ni jambo la kheri kwa mchezaji wake kuimarika kwa afya yake.

“Samatta amekuwa akifanya mazoezi binafsi na hata yale ya gym,  goti lake linaendelea vizuri na anaweza kurejea Desemba hii mwishoni,” alisema. 


Kuhusu Thomas Ulimwengu ambaye naye ni majeruhi, Kisongo alisema: “Ulimwengu naye anaendelea vizuri, tunasubiri Januari tuone anaelekea wapi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic