December 1, 2017




Kampuni ya Star Media (T) Ltd inayomiliki nembo ya StarTimes wakishirikiana na Kampuni ya Ubashiri wa Matokeo ya Michezo, Princess Bet, usiku wa Desemba Mosi, mwaka huu waliwezesha wapenzi wa soka kutazama moja kwa moja matangazo ya upangaji wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia litakalofanyika Urusi, Juni mwakani.

Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Princess Casino jijini Dar es Salaam.


Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Uhusiano wa StarTimes, Juma Suluhu alisema: "Tumejikita katika kuhakikisha kila Mtanzania anaangalia taarifa, burudani na maudhui yote muhimu duniani ndiyo maana tunawaletea Kombe la Dunia mpaka nyumbani. Hafla hii ya leo ni kielelezo tosha ya niyasemayo."

Suluhu maarufu kama Sharobaro aliongeza kuwa wametoa ofa ya Krismasi ambapo wamepunguza bei ya king'amuzi cha antena kutoka 47,000 na kuwa 34,000 huku bei ya Dikoda ya Combo iliyokuwa Sh 86,000 sasa ni Sh 78,000 ambapo utapatiwa dish na kifurushi cha mwezi mmoja bure. 








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic