December 29, 2017



Siku chache baada ya kufungashiwa virago na Klabu ya Simba, aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog amepata dili nchini Sudan.

Omog ambaye hivi karibuni alifungashiwa virago na Simba kutokana na kushindwa kuiongoza timu hiyo kupata matokeo mazuri katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Green Warriors amepata dili katika Klabu ya Al-Merreikh ambayo ni moja kati ya miamba ya soka nchini Sudan.

Juzi Jumatano, Al-Merreikh ilimtumia barua pepe Omog ya kumtaka akajiunge na timu hiyo kutokana na kuvutiwa na utendaji wake wa kazi wakati alipokuwa akiitumikia Simba lakini pia wasifu wake alionao katika soka la Afrika.

Habari za kuaminika zinaeleza inadaiwa kuwa baada ya barua hiyo Omog aliwajibu na kuwataka wampatie muda wa mwezi mmoja ili aweze kwenda kwao Cameroon na kuweka mambo yake sawa.

“Omog anatarajia kuondoka nchini Jumamosi endapo atamalizana na uongozi, lakini jana (juzi) amepokea barua pepe kutoka Sudan katika Klabu ya Al-Merreikh ikimhitaji akawe kocha mkuu wa timu hiyo.

“Hata hivyo, aliijibu barua hiyo na kuwaambia wampatie muda kwanza aende kwao akaweke mambo yake sawa,” kilisema chanzo hicho cha habari na kuongeza:


“Pia ukiachana na dili hilo, huko kwao nao wamemuita ili akakabidhiwe majukumu katika timu yao ya taifa kwa ajili ya michuano ya AFCON ya mwaka 2019.”

SOURCE: CHAMPIONI 

1 COMMENTS:

  1. Sasa kama Omog ana dili au anatakiwa na Almereikh ya sudani sisi kama watanzania na Simba inatusaidia nini? Sisi kama watanzania na waandishi wa habari ambao kwa kiasi kikubwa tunatakiwa kutoa maoni yetu kuishauri Simba kuangalia mbele zaidi na kusahau ya Omog kwa sasa kwani ya Omog yameshapita. Hata Omog angekaa simba miaka mia moja zidi ijayo lakini ipo siku angeondoka tu na kuiacha Simba ya Tanzania na watanzania wake. Viongozi na wanachama wa Simba sio wapumbavu ninaimani wapo katika mchakato wa kumpata mtu sahihi zaidi wa kuikochi Simba atakaeleta maendeleo chanya zaidi kwa klabu ya Simba na Tanzania kwa ujumla. Tena niseme tu yakwamba Tanzania tulishachelewa zamani tu katika masuala ya mpira. Tunahitaji viongozi na makocha wa spidi ya haraka zaidi ili ku catch up na wenzetu waliotutangulia Africa. Spidi ya Omog haionekani yakuwa ya kisasa na haraka zaidi kwa mazingira ya mpira wa Tanzania. Pengine Omog anaweza kufanya vizuri zaidi Africa kusini kuliko Tanzania au angeweza kufanya vizuri zaidi na Timu ya Taifa ya Tanzania kuliko Salum Mayanga. Kwa Simba kumkatisha mkataba Omog wapo sahihi tu ninaimani muda si mrefu itathibitika na kuwaziba vidomo vidomo wanafiki yakwamba kweli walikuwa wapo sahihi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic