December 15, 2017



Kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, imeshindwa kuendelea kufuatia kukwama kwa nyaraka za ushahidi zinazodaiwa kuwa kwenye ofisi nyingine ya Aveva.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani.

Katika kesi inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Makahama ya Kisutu, Victoria Nongwa, jana iliitwa kwa ajili ya kutajwa ambapo Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai ameiambia mahakama hiyo kuwa jalada la kesi hiyo limeshatoka kwa DPP na kurudishwa Takukuru kwa ajili ya kurekebisha sehemu ya upelelezi ikiwemo suala la kutaka kufanya uchunguzi katika ofisi  nyingine ya mshitakiwa namba moja kitendo kilichowashangaza.

Swai alisema kuwa kwa sasa jalada la kesi hiyo lipo  mikononi mwa Takukuru baada ya kutoka kwa DPP kwa ajili ya kuendelea na dosari walizoambiwa wazirekebishe baada ya kugundua Aveva kuwa na ofisi mbili, hivyo walimuandikia barua kwenda gerezani kwa ajili ya kuweza kutoa funguo ili uchunguzi uweze kuendelea.

"Jalada kwa sasa lipo mikononi mwa Takukuru kwa ajili ya kurekebisha baadhi ya dosari tulizoambiwa na DPP kwa sababu tumebani kuwa mshtakiwa namba moja akiwa mhusika mkuu kuwa na ofisi mbili ambazo zote alikuwa akizitumia katika shughuli zake na kwenye hizo ofisi ndiyo zipo baadhi nyaraka ambazo tunahitaji ili tuweze kuendelea na kesi.

"Tumeshamuandikia barua kupitia magereza kwa sababu yeye ndiyo ana uwezo wa kuidhinisha kupatikana kwa funguo ili tuweze kufika huko lakini inashangaza yeye pekee kuwa na ofisi mbili tofauti kwa mpigo ila kwa upande wa magereza bado hawajatujibu hivyo tunaomba tarehe nyingine," alisema Swai.

Hata hivyo upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na na wakili, Evodius Mtawala tayari wameipata barua hiyo na wanachokifanya ni kukusanya nyaraka zote zinazohitajika kabla ya kuwapa ili kesi hiyo ianze kusikilizwa ambapo hakimu Nongwa amesogeza mbele kesi hiyo hadi Desemba 28, mwaka huu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic