Klabu ya AFC ya Sweden imeendelea inamtaka kiungo Said Hamis Ndemla lakini imesisitiza haina fedha za kulipa badala ya mkataba wa makubaliano.
Mmoja wa maofisa wa AFC amesema, watamchukua Ndemla iwapo Simba watakubali kuingia mkataba unaoweza kuwafadisha mbeleni.
"Fedha za kulipa kama kumnunua hatuna, Simba wanajua unaweza kuzungumza nao," alisema kutoka Sweden.
"Waulize wakueleze vizuri lakini sisi wakikubali tutamchukua na kumlipa mshahara mzuri na akipata nafasi ya kucheza akauzwa, basi tutagawana kwa mujibu wa makubaliano.
"Said (Ndemla) bado ni mchezaji kinda, bado ana CV ndogo na tunahitaji kumkuza na gharama zitakuwa zetu si za Simba."
Ndemla alifanya majaribio katika klabu hiyo na kufanikiwa lakini inaonekana Simba na AFC bado hawajafikia mwafaka katika suala la manunuzi.
SIMBA SIMBA SIMBA....TUSIANGALIE FEDHA TUANGALIE MAISHA:::
ReplyDeleteNaamini Simba FC ni waelewa sana..hawawezi kumfanya Said Hamis Ndemla asijumuike katika timu inayomtaka. Tumuache aende akaangalie maisha mengine. Kitu cha Msingi ni ni kufanya makubaliano ya kimaandishi. watuambie kama asipouzwa tuwape miaka mingapi watulipe pesa. Ndemla bado ni mchanga anahitaji kupata uzoefu zaidi. Kwa kiwango anachoonesha ni mchezaji muhimu angalau sisi hatuoni nini anachokifanya...ndio maana hata timu ya Taifa tunamuacha..wenzetu wazungu waliotupita katika fikra wameliona hilo. Wapo tayari kumlipa mshahara ila hela za kumununua hakuna. Kikubwa ni maisha ya mchezaji mwenyewe..nao wameligundua ndio maana wakatanguliza "tutamlipa mshahara mzuri".
Je Simba SC wenzangu mmewaza nini juu ya hilo???msiwaze kupata hasara maana tayari zaidi ya Misimu mitatu hadi minne anatumikia timu hii. Kwahiyo hata hasara kashazifidia muda mrefu.Kikubwa ni kujua..Je yeye mwenyewe yupo tayari kwenda Sweden???kama yupo tayari tufanye Confirmation za Said kwenda huko.
Niwaombe viongozi wa Simba wajifikilie mara mbili mbili...najua si watu wa kuminya wachezaji. Tumtoe mtoto nae aende akacheze.