Kocha Arsene Wenger wa Arsenal, ndiye kocha anayeongoza kwa kulaumiwa zaidi na kwa muda mrefu kuliko wote England. Je, unafikiri ndiye mkosaji zaidi katika kikosi hicho, au wachezaji wake wanamuangusha?
Yote yanawezekana kwamba inawezekana kwa sasa mbinu anazotumia mzee Wenger zikawa sio rafiki kwa mazingira ya ligi ya Uingereza lakini pia inawezekana wachezaji wanamuangusha, suala la mbinu inaweza ikawa ndo sababu kubwa ya Arsenal kufanya vibaya maana ukiangalia kwa mfumo anaotumia wa 3-5-2 unahitaji viungo wanaojituma sana na kuelewa majukumu yao vizuri,ukiangalia tangu kuondoka kwa akina Patrick Vieira na baadae Gilberto hakujatokea viuongo wakabaji wazuri tena pale Arsenal, kwa kutunza heshima yake ni bora atafute timu nchi nyengine ya kufundisha inaweza ikawa na mafanikio makubwa kwa mbinu zake maana akisema auze wachezaji na kununua wengine watakaoendana na matakwa ya mfumo wake inaweza kumchukua muda mpaka kikosi kuja kukaa sawa na kama tulivyoona akishajenga kikosi kabla hakijafika kwenye mafanikio wachezaji wanataka kuondoka mfano kwa Sanchez na Ozil kwa sasa. Ni kocha mzuri ila atafute tu changamoto nchi nyengine Uingereza pameshakuwa pagumu kwake na atazidi kufedheheka.

ReplyDelete