January 30, 2018



Ule ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC umeamsha morali katika kikosi cha Yanga.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, anaamini wamerejea katika ile hali yao na wana nafasi ya kuendelea kufanya vema.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam, Complex,  Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo sasa wamefikisha pointi 28 wakiwa nafasi ya tatu, nyuma ya Azam wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 30, wakati vinara wa  ligi hiyo, Simba, wakiongoza kwa pointi 32.

Yanga ilionyesha kiwango kizuri katika mechi hiyo na kufanikiwa kutoka nyuma kwa bao moja na kusawazisha kabla ya kufunga la ushindi.

“Tuliwaambia wachezaji wetu warudi nyuma na watulie ili tuweze kwenda sawa na kasi yao, na kweli tuliweza kupata bao la kusawazisha na la ushindi na sasa tumerejea kwenye njia yetu ya kuendelea kupambana  licha ya ligi ya msimu imekuwa na changamoto ya ushindani mkali tofauti na hapo nyuma.

“Matokeo hayajabadilisha nafasi yetu kwenye msimamo wa ligi kwa zile timu tatu za juu isipokuwa tumepunguza nafasi ya pointi na timu ambayo tumecheza nao kwa sababu siku zote ukitaka kuwa bingwa lazima umfunge unayeshindana naye, hivyo malengo yetu bado yapo vilevile,” alisema Nsajigwa.

Yanga imekua ikisuasua kutokana na kuandamwa na wachezaji wake wengi ambao ni majeruhi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic