January 6, 2018



Ili kuhakikisha wateja wake wanapata ikiwezekana zaidi ya kile wanacholipia, kwa mara nyingine King’amuzi cha DStv kupitia chaneli yake ya Maisha Magic Bongo (MMB) imeleta mapinduzi katika Tasnia ya Filamu nchini kwa kuongeza tamthilia mbili ili kuwahakikishia Watanzania na wateja wake wanapata burudani zaidi.

Tamthilia hizo mpya ni Sarafu na Kapuni ambazo zilizinduliwa na Waziri Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Harison Mwakyembe pamoja na maofisa mbalimbali wa wadau wa filamu nchini katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Kwa mara ya kwanza tamthilia hizo, zitaanza kurushwa hewani kuanzia wiki ijayo katika DStv chaneli 160 ya Maisha Magic Bongo.

Akielezea tamthilia hizo mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Maharage Chande alisema kuwa Kapuni ni tamthilia iliyoandaliwa na Mtanzania Leah Mwendamseke na imesheheni vituko na misukosuko ya mahusiano, usaliti wa kimapenzi unaoleta chuki, uhasama na uadui mkubwa.

Maharage alisema, tamthilia hiyo imeigizwa na waigizaji maarufu kama Jacquline Wolper, Gabo, Kajala, Masanja, Jenifer Kyaka ‘Odama’, Mwanamuziki Quick Rocka, Dj Rommy Jones na mastaa wengine wengi.

Alisema Tamthilia ya Sarafu iliyoandaliwa na John Isike, ni maridadi na imebeba marafiki wawili ambao wanaingia kwenye chuki na uadui mkubwa mpaka kuingiza familia zao kwenye hatari kisa kikiwa ni fedha zinazozaa kiburi dharau na anasa za kupitiliza.

Waigizaji wa tamthilia hiyo ni Mohammed Funga Funga ‘ Mzee Jengua’, Mzee Chilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Hemed Suleiman, Irene Uwoya, Idris Sultan, Yusuph Mlela na mastaa wengine.


Akizungumzia uzinduzi huo, Mwakyembe alisema: “Niwataka wasanii hapa nchini kuhakikisha  wananufaika na kazi zao za sanaa na kwamba serikali kwa dhamana iliyonayo itakuwa tayari muda wowote kushirikiana na wasanii kuhakikisha wanapata haki zao kutokana na kazi zao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic