January 29, 2018

KAIMU KATIBU MKUU WA TFF, WILFRED KIDAO


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeamka kutoka usingizini na kutoa angalizo katika mechi za mwisho za Daraja la Kwanza.

Katika makundi matatu ya ligi hiyo, zinatakiwa kupanda timu sita lakini hadi sasa imepanda moja tu ya JKT Ruvu kutoka Kundi A.

Kundi A, bado halijapata timu ya pili na makundi mawili ya B na C, haijajulikana timu ipi imepanda.

Kutokana na hali hiyo, TFF imetoa angalizo na kusema inafuatilia nyendo za wachezaji, viongozi na waamuzi ambao watajaribu kupanga matokeo katika mechi za mwisho.

TFF imesisitiza kwamba atakayebainika kupanga matokeo mara moja atachukuliwa hatua za kisheria na zitakuwa ni kali.

Kutokana na timu tano zote kutakiwa kupanda siku ya mwisho, kumekuwa na hofu kubwa ya suala la upangaji matokeo kutokea.


Tayari SALEHJEMBE ilishaiionya TFF kuhakikisha iko macho katika siku ya mwisho ya ligi hiyo ili kueousha upangaji wa matokeo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic