Timu ya Singida United inayonolewa na Hans van Der Pluijm, raia wa Uholanzi, imeweka rekodi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar baada ya kushinda mechi zote nne na katika mechi hizo kutoa wachezaji bora wa mechi.
Singida United ambayo ipo Kundi B kwenye michuano hiyo, imeshatinga nusu fainali pamoja na Yanga, huku Azam nayo kutoka Kundi A ikiwa imefuzu ikisubiriwa timu moja kutoka kundi hilo kati ya Simba na URA.
Katika mechi hizo nne, Singida United imezifunga Zimamoto mabao 3-2, Taifa Jang’ombe (3-1), Mlandege (3-0) na JKU (2-0) ambapo Salit Kambale, Danny Usengimana, Mudathir Yahaya na Deus Kaseke wakifanikiwa kuchaguliwa kuwa wachezaji bora.
Leo Jumatatu timu hiyo inamaliza mechi yake ya mwisho ya makundi kwa kucheza na Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment