Kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko ameendeleza matumaini ya kurejea baada ya kuendelea na mazoezi ya taratibu.
Kamusoko raia wa Zimbabwe ambaye amekaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu sasa, ameendelea na mazoezi akizunguka uwanja wakati Yanga ilipokuwa ikijifua kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Matumaini ya kurejea kwa kiungo huyo muhimu wa Yanga yanatokana na namna hali yake inavyozidi kuimarika namna anavyoendelea na mazoezi.
Hata hivyo, bado hajaanza kugusa mpira badala yake ametakiwa kuendelea kuimarisha viungo vyake.
WAKATI KAMUSOKO ANAONESHA MATUMAINI WENGINE HAWATAMANI:
ReplyDeleteMoja ya kitu nilichofurahi kuona ni Beno Kakolanya kurudi na kuanza mazoezi na wenzake. Hii inaonesha ni jinsi gani seriousness imeanza kutawala baada ya mashindano ya Mapinduzi pale Unguja. Vijana wameanza kufanya mazoezi kwa pamoja na naamini timu itarudi baada ya siku si nyingi. Kilio changu ni uwezo wa kipa namba moja Rostand hauwezi kumshawishi mtu ila naamini kwa Beno na Kabwili.
Udhaifu aliouonesha Rostand kwenye mashindano ya mapinduzi yamempunguzi kredit kwa jamii ya mpira nchini. Ajue Yanga si African Lyon....hii ni timu inayohitaji kitu na si kubweteka. Kingine sioni sababu ya kuwa na kipa kutoka nje wakati watu wetu wapo vizuri zaidi. Tumpe nafasi au tuwape nafasi vijana wetu kwenye hiyo nafasi.