January 9, 2018


Mashabiki mbalimbali wa soka wameongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Kikwete katika mazishi ya nyota wa zamani wa Taifa Stars, Athuman Juma ‘Chama’.

Pamoja na Kikwete, katika makaburi ya Kisutu jijini Dar, Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ni kati ya watu waliojitokeza katika mazishi ya Chama wakiungana na waombolezaji wengine pamoja na Kikwete.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambaye ni mwanamichezo, pia alikuwa kati ya waliofika kumzika Chama.

Chama aliyefariki dunia juzi baada ya kuugua kwa muda mrefu, alikuwa kati ya nyota waliong’ara na Pamba ya Mwanza na Yanga pia timu ya tafa, Taifa Stars.

Viongozi, mashabiki, wanachama na wanasoka mbalimbali wa zamani wa Yanga, Simba na timu nyingine walijitokeza kwa wingi wakiungana na wadau wengine kumsindikiza Chama katika safari yake hiyo ya mwisho.

Zamoyoni Mogella ambaye alikuwa mshambuliaji aliyazuiwa na Chama hadi kusababisha ule msemo wa “Chama na Mogella” alikuwa kati ya watu waliojitokeza hii leo.












0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic