January 14, 2018


HII NI KWA TAARIFA YAKO TU, BASI LA AZAM PEKEE NDIYO LIMEONDOKA KWA SHANGWE,  NIDHAMU

SImba, Yanga na Azam FC zote zilipitia bandari ya Dar es Salaam kwenda na kurudi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Timu pekee ambao siku ya kupokelewa walirejea na furaha na kuonyesha nidhamu sahihi ni Azam FC wakiwa wamebeba Kombe la Mapinduzi walilolitwaa kwa kuwafunga URA ya Uganda.

Simba walioanza kutolewa mapema, walirejea na kupokelewa na basi laeo lakini wachezaji wengi wakapanda bodaboda, bajaj na kuelekea makwao au wanapojua.

Walifuatia Yanga waliiotoka katika nusu fainali, nao waliingia kwenye basi lao ingawa ilikuwa tafrani, mashabiki wakionyesha jazba huku wakiandika mapango kuwashutumu baadhi ya wachezaji wao.

Azam FC wao walifika na kwa utaratibu sahihi wakaingia ndani ya basi, baada ya mipangilio yao kwenda kama ilivyotakiwa, basi likaondoka taratibu likiwa na wachezaji wote ndani.







1 COMMENTS:

  1. KWA TAARIFA YAKO....:
    Simba na Yanga hapa nchini ndio timu zenye washabiki na wapenzi wengi kuliko Timu zingine. Na kwa taarifa yako..timu hizi ndizo zinzotumika kuuza na kusaidia Blog nyingi za michezo kutazamwa. Siku Yanga au Simba isipokuwa kwenye taarifa za chombo chochote ujue kitakosa mvuto. We angalia hata mashamsham ya Kombe la Mapinduzi hayakuwa makubwa baada ya hizi timu kutolewa.

    Timu hizi ndizo pekee ambazo huwa zinaombeana mabaya hasa kwa washabiki wake. nikwambie sasa....Simba walijizomea wenyewe ila Yanga walizomewa na mashabiki wa Simba ambao hawakutaka Timu ya Yanga ifike mbali katika mashindano hayo.

    Simba SC washabiki wake walipata kadhabu baada ya kutolewa mapema nje ya matarajio yao. Baada ya hapo ili kupoza machungu wakaona heri wamalizie hasira zao kwa Yanga baada ya kutolewa. Ukiangalia Kikosi bora kwa sasa...Simba ina kikosi bora lakini kimekosa muunganiko mzuri...Yanga ina kikosi cha Wastani ambacho ni kidogo kuliko hata cha Singida United au Azam FC. Azam ina kikosi cha vijana wanaotaka makubwa yaani wenye hari ya uhitaji wa mafanikio...ila hawana kikosi bora.

    Kwahiyo kutopata mapokezi mazuri kwa timu kama Simba ni kutokana na wenyewe kutofanya vizuri kwenye mashindano hayo iliyoleteleza washabiki wao kupatwa na jazba. Washabiki wa Yanga maumivu yao ni kukosa kwa penati ila matarajio yao hayakuwa hata hapo walipofika. Waliamini watatoka mapema zaidi katika mashindano kutokana na ufinyu wa kikosi chao.

    ACHA WAKUBWA WABAKI KUWA WAKUBWA HATA MAISHA YAKIGEUKA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic