January 23, 2018
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustin Ollomi amesema aliyeshambuliwa na Juma Nyosso amepata jeraha la kupasuka usoni.

Ollomi amesema jeraha hilo limetokana na yeye kupigwa kifuti na Nyosso na kuzimia mara tu baada ya Kagera Sugar kufungwa kwa mabao 2-0 na Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, jana.

“Wakati mechi imeisha na watu wanatoka nje, yule shabiki alikuwa na Vuvuzela, inaelezwa ni shabiki wa Simba na alikuwa akienda anapuliza mbele ya Nyosso ambaye aliingiwa na hasira.

“Kutokana na hasira hizo, Nyosso alimshika yule shabiki na kumpiga namna hii kwa kifuti na kumjeruhi kwenye pasi la uso,” alisema.


Nyosso alipelekwa kituoni baada ya tukio hilo ambalo limekuwa gumzo zaidi mara baada ya mechi hiyo ambayo Simba walishinda kwa kupata kwa mabao mawili yote katika kipindi cha pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV