January 17, 2018





Siku ya Jumatatu ya Januari mosi, 2018, mamilioni ya mashabiki wa soka kote duniani waliokuwa wakitazama mtanange wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Everton na Manchester United, walipata fursa ya kushuhudia jambo kubwa sana na la kihistoria.

Katika siku hiyo ya kwanza ya mwaka mpya, Everton chini ya kocha wao Sam Allarydies walikuwa wenyeji wa Manchester United kwenye dimba la Goodison Park.

Everton ambao wanadhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa, hawakuvaa jezi yenye nembo ya mdhamini wao huyo kama ilivyo ada, na badala yake walivaa jezi yao maarufu ya bluu yenye maneno ya kuhamasisha kampeni ya ‘Kits For Africa’ inayoweza kutafsiriwa kama “Vifaa vya Michezo Kwa Afrika.”

‘Kits For Africa’ ni nini?
Kits For Afrika ni kampeni iliyoanzishwa na kampuni ya SportPesa ikiwa na lengo la kuhamasisha wachezaji na mashabiki wa klabu wanazozidhamini barani Ulaya kuchangia vifaa vya michezo kwa wachezaji na timu za ngazi za chini barani Afrika zenye uhitaji huo.

Sote tutakuwa ni mashahidi jinsi ambavyo mpira wa miguu kwa bara la Afrika unakumbwa na changamoto ya vifaa ya michezo vyenye ubora kama vile jezi, viatu, soksi n.k
Kwa kulizingatia hilo, SportPesa iliona umuhimu wa kuwatumia washirika wake barani Ulaya kama vile klabu ya Hull City, Southampton na Everton za nchini Uingereza kwa ajili ya kuwezesha uchangiaji huo.

‘Kits For Africa’ ilianza kama Kits For Kenya mwaka 2016 ambapo mashabiki wa klabu ya Hull City walikusanya vifaa mbalimbali vya michezo kwenye uwanja wao wa nyumbani wa KCom ambapo vifaa hivyo vilitumwa nchini Kenya Desemba 2016 na kupelekwa moja kwa moja katika eneo la Korogocho jijini Nairobi.

Baada ya SportPesa kutanua wigo wake wa kibiashara nchini Tanzania, ndipo kukawa na umuhimu wa kampeni hiyo kuwa mahsusi kwa bara zima la Afrika ambapo SportPesa inaendesha shughuli zake.

Januari Mosi
Mechi ya Januari mosi kati ya Everton na Manchester United iliyopigwa dimbani Goodison Park, ilikuwa ni kilele cha ukusanyaji wa vifaa hivyo kwa upande wa klabu ya Everton ambao walipokea kampeni hiyo kwa mikoni miwili kutokana na mahusiano mazuri waliyonayo na bara la Afrika kwa sasa.

Katika mechi hiyo, mashabiki walikusanya jezi, soksi na viatu vya mpira kwenye sehemu zilizotengwa maalum uwanja hapo ambapo zaidi ya jozi 4000 za vifaa zilikusanywa katika kuhitimisha zoezi hilo ambalo lilianza kuendeshwa rasmi Desemba mwaka jana.

Ni fahari kwetu
‘Kits For Africa’ ni kampeni ambayo imepokelewa vyema na wachezaji pamoja na mashabiki wa klabu hiyo huku wakiamini kwa dhati kuwa watatoa mchango wao kwa bara la Afrika ili kutimiza ndoto za waafrika wengi kama anavyosema Mkuu wa kitengp cha biashara wa Everton FC, Alan McTavish.

“Tuna shauku ya dhati ya kufanya kazi kwa ukaribu na wadhamini wetu wakuu, SportPesa kwa ajili ya kampeni ya ‘Kits For Africa’. Ni jambo la kutia moyo kuona wana familia wa Everton wakiunga mkono kampeni hii ili kusaidia soka la ngazi za chini barani Afrika.”

Naye Leon Osman amefarikijika na kampeni hiyo huku akitoa ushahidi wa kile alichokiona nchini Kenya alipoenda kuzindua kampeni hiyo rasmi.

“Nimekutana na watu wengi Nairobi ambao wana mapenzi na mpira wa miguu lakini wengi wao hawawezi kucheza kwasababu hawana vifaa. Ni muhimu kwetu kuwachangia vifaa ili kuwasaidia wachezaji wanaochipukia kutimiza ndoto zao,” alisema.

Walengwa
Hakika kampeni hii imekuwa yenye mafanikio makubwa kwa ushirikiano na Everton hasa ukizingatia kuwa kampeni hiyo imeweza kuwafikia watu zaidi ya milioni 3.6 kwenye mitandao ya kijamii ya klabu ya Everton bila kusahau mamilioni ya watu waliotazama mechi ile kupitia vituo mbalimbali vya luninga duniani kote.

Vifaa hivyo vitatumwa barani Afrika hivi karibuni ambapo SportPesa wataongoza zoezi zima la kuhakikisha vinawafikia walengwa popote walipo na hakika vifaa hivyo vitasaidia kuongeza msisimko wa soka barani Afrika kwa wachezaji chipukizi na wale wenye mapenzi ya dhati na soka kama anavyohitimisha Mlinzi wa kati wa klabu ya Everton, Michael Keane.

“Ni muhimu kwa Everton na SportPesa kufanya jambo kama hili. Ni vizuri kuona mashabiki wakichangia viatu na jezi kwa wale ambao wana mapenzi na mpira wa miguu. Tunaona fahari kubwa kuwa sehemu ya ‘Kits For Africa’ na naamini tutaleta mabadiliko.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic