February 28, 2018


Na George Mganga
 
Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, ameendelea kutoa msisitizo wake kuwa bado hampi nafasi Golikipa Youthe Rostand kuendelea kusalia langoni.

Akilimali amesema uimara wa kipa huyo umepotea kutokana na hivi karibuni kiwango chake kushuka hivyo si wakati mwafaka wa kuendelea kumtumia.

Aidha Akilimali ameeleza ifikie wakati sasa benchi la ufundi limpe nafasi Beno Kakolanya na Ramadhan Kabwili ya kucheza kuliko kuendelea kusalia benchi.

"Mimi nimeona ameshuka kiwango chake kwa muda mrefu sasa, sioni haja ya kuendelea kuwa kipa katika klabu yetu, nadhani ifike hatua sasa vijana Ramadhan Kabwili na Beno Kakolanya wapewe nafasi ya kucheza nafasi yake" amesema Akilimali.

Yanga ipo mkoani Mtwara leo kucheza dhidi ya Ndanda FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

2 COMMENTS:

  1. Huyu mzee kama ana koz ya ukocha.. tunaomba aende akaiokoe Njombe mji wasishuke daraja.. au akawapandishe toto africa ligi kuu.
    Amekuwa bench la ufundi sik hz

    ReplyDelete
  2. Maneno ya Mzee wetu ni maoni yake binafsi na wakati fulani yana ukweli lakini hata Kakolanya au Kabwili nao ni binadamu tu kama ni makosa nao wanayafanya wakiwa uwanjani. Bado Rostand ni mzuri na imara na kwakweli makipa wote 3 ni wazuri ni kupeana zamu tu ya kutumikia kulingana na maamuzi ya Kocha na benchi lake la ufundi. Sio busara kuwaingilia makocha kazi ya kupanga wachezaji. Tutoke huko.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic