OKWI APEWA ASILIMIA KUBWA YA KUCHEZA DHIDI YA STAND, TAARIFA IKUFIKIE
Na George Mganga
Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi, ana uwezekano mkubwa wa kucheza mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United utakaopigwa Ijumaa ya Machi 4 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba katika kurasa za mitandao ya kijamii jana Jumanne, Daktari wa timu, Yassin Gembe, amesema hali ya mchezaji huyo inaendelea vizuri na kuna asilimia kubwa ya kucheza Ijumaa.
''Okwi anaendelea vizuri sana tofauti na jana, kwa hali aliyonayo pamoja na tiba ambazo tumeshampatia ni asilimia kubwa sana kwa yeye kuwepo kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Stand United Ijumaa hii'' alisema Gembe.
Okwi aliumia katika mchezo uliopita dhidi ya Mbao FC katika ligi, na kupelekea kutolewa nje huku nafasi yake ikichukuliwa na Laudit Mavugo.
Mpaka sasa Okwi amefunga jumla ya mabao 16 katika michezo 19 ambazo Simba imecheza mpaka sasa katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment