Ruvu Shooting sasa wanakwenda na mtindo wa "Kupapasa" na anayechungulia, wao wanapiga tu. Hayo ni maneno ya Msemaji wao, Masau Bwire.
Kuonyesha kwamba wako vizuri, leo hii Ruvu Shooting inayodhaminiwa na Hawaii Product inayotengeneza maziwa ya Cowbell, leo imezindua jezi zake zitakazotumiwa na mashabiki.
Katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Happines Willium Seneda ambaye ni Mkuu wa Wilaya Kisarawe, alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Injinia Evarist Ndikilo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, mkuu huyo wa wilaya alisema ni jambo zuri limefanywa na Ruvu Shooting hivyo wanapaswa kuungwa mkono.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Ruvu Shooting, Meja Michael James alisema timu yao hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002 na kucheza ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu wa 2005/06 imekuwa ikipambana kuhakikisha inaleta mapinduzi ya soka hapa nchini.
Meja James aliongeza kuwa kuendesha timu ni gharama kubwa hivyo udhamini wa Azam TV na Vodacom pekee hautoshi lakini kuongezeka kwa udhamini wa Cowbell unawafanya kujiendesha vizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment