February 26, 2018


Na George Mganga

Mshambuliaji wa klabu ya Simba, John Bocco, ataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara Jumatatu ya leo, wakati timu yake itakapokutana na Mbao FC ya jijini Mwanza.

Bocco ataikosa mechi ya leo kutokana na majeraha ya mguu wake, aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu uliopita, February 25 2018, dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Mbali na kuukosa mchezo huu, Bocco pia hakuwepo katika kikosi cha Simba kilichocheza mechi ya Kombe la Shirikisho Africa dhidi ya Gendarmarie Nationale FC ya Djibout ambao Simba walishinda bao 1-0.

Hii itakuwa mechi ya pili sasa Bocco anakosekana dimbani baada ya Gendarmarie, na leo dhidi ya Mbao FC.


1 COMMENTS:

  1. Hatuelewi madhara tunayowasababishia wachezaji wetu mastaa kwa kuruhusu faulo za kukamiana zisizo za kimchezo. Marefarii wetu na TFF umefika wakati muangalie namna bora ya kuwalinda wachezaji wetu wasiumizwe ovyoovyo kwa makusudi na wachezaji wenzao kwenye mechi. Wachezaji wote tu awe Yanga, Simba, Azam, Mtibwa, Ruvu wote walindwe ipasavyo na marefarii wetu ndani ya mchezo uwanjani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic