February 26, 2018



Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage, amesema kuwa hakuna kitu kitakachoizuia timu hiyo kutangaza ubingwa mapema msimu huu.

Simba inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 42, huku Yanga wakiwa na pointi 37, wakiwa wametofautiana pointi tano tu lakini Rage amesisitiza kuwa kama Simba hawatabweteka, mapema tu watatangaza ubingwa.

“Simba ina nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa iwapo haitabweteka, timu nyingi kwa sasa zina udhamini wa kutosha, hivyo kusababisha ushindani kuwa mkubwa kwenye ligi, hivyo hawapaswi kuridhika na matokeo.

“Wachezaji wanatakiwa watambue kwa sasa wana jukumu moja tu la kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, timu ambayo ilikuwa inatishia kidogo ilikuwa Azam lakini kwa sasa yenyewe haipo vizuri sana, hivyo bado inayo nafasi ya kufanya vizuri.


“Ushindani jinsi ulivyo hakuna aliyetegemea Mbao ingetolewa na Njombe Mji kwenye FA, wachezaji wa Simba wasibweteke hata kidogo, waonyeshe nguvu ya kuweza kufanya vyema kwenye ligi,” alisema Rage.

SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Kabisa Rage yupo sawa Simba inauwezo wakutangaza ubingwa mapema lakini ligi ipofikia sio uwezo wa mpira peke yake utakaoweza kuingusha Simba bali fitna za ndani na za nje ya uwanja kutoka kwa wanaowatakia mabaya ndio hatari zaidi. Kwa mfano mechi ya leo Simba hachezi na Mbao peke yake bali yanga lazima watakuwa wanahangaika kuhakikisha Simba wakapoteza hii mechi. Kuna wachezaji wa Mbao wanaotafuta soko la ajira lenye maslahi zaidi watapigana kijihadi kuwashawishi wanaohusika na masuala ya usjili lakini itakuwa ni jambo la kushangaza kwa wachezaji wa Simba kuwaruhusu wachezaji wa Mbao kuuthibitishia Umma kuwa wao ndio wenye uwezo wa kuichezea simba na si wale wanaoituimikia sasa. Si dhani kama wachezaji wa Simba wapo tayari kudhalishwa nyumbani kwao mbele ya mashabiki wao.

    ReplyDelete
  2. Simba hakuna kubweteka hakikisheni mechi zote zilizobakia mnashinda tena kwa bao nyingi tu safari hii hakikisdheni pengo la pointi linaendelea kuwepo mpaka mwisho. Uwezo mnao Simba acheni kudharau mechi yeyote chezeni kwa nguvu moja mpaka mwisho ubingwa wenu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic