CONTE AZIDI KUJIWEKEA MAZINGIRA MAGUMU KUBAKIA CHELSEA, AKUNG'UTWA 2-1 NA MANCHESTER
Hali ya Antonio Conte kuendelea kusalia Chelsea imezidi kuwa ngumu baada ya timu yake kupokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu.
Mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Old Trafford, Chelsea ndiyo walikuwa wa kwanza kuanza kuliona lango la Manchester United kwa kupata bao la kwanza kupitia Willian katika dakika ya 32 tu ya mchezo.
Hata hivyo bao hilo halikudumu, kwani ilichukua dakika 9 pekee kwa Man United kusawazisha kupitia Romeru Lukaku kwenye dakika ya 39 ya mchezo.
Bao la Lukaku liliufanya mchezo kwenda sare ya bao 1-1 katika kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilileta neema upande wa Man United, ambapo Jesse Lingard, aliongeza msumari wa pili kwenye dakika ya 75 na kufanya matokeo yaende mpaka kipyenga cha mwisho yakiwa 1-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment