February 25, 2018


Na George Mganga

Mtibwa Sugar imekuwa miongoni mwa timu zilizoingia hatua ya nane bora ya mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuisambaratisha Buseresere FC kwa mabao 3-0.

Katika mchezo huo uliopigwa Nyamagana Stadium, Mtibwa Sugar walijipatia mabao yao kupitia Hassan Dilunga, aliyefunga kwa njia ya penati katika dakika ya 52, na katika dakika ya 80, Haruna Chanongo aliandika bao la pili.

Haikuchukua muda mrefu, kuelekea mwishoni mwa mchezo, kiungo Ally Malani, aliiongezea Mtibwa bao la 3 kwenye dakika ya 90 na kuufanya mchezo huo umalizike kwa matokeo ya 3-0.

Sasa Mtibwa inasubiri droo ya kupangiwa icheze na nani katika hatua ya robo fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic