February 18, 2018


Kikosi cha Simba kimekwea pipa kwenda Djibouti kikipitia Nairobi nchini Kenya, hii ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Simba inakwenda Djibouti kucheza mechi yake ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Gendamarie.


Katika mechi ya kwanza, Simba ilishinda kwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa Simba wameondoka mafungu mawili kwa Kenya Airways na watakutana Nairobi kabla ya kupanda ndege moja kwenda Djibouti

Kutoka Dar es Salaam hadi Nairobi ni muda wa saa moja na dakika 15 na Nairobi Djibouti ni saa mbili na dakika 45.











0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic