February 18, 2018



Wakati kikosi cha Simba kimekwea pipa kwenda Djibouti kuivaa Gendamarie katika mechi ya Kombe la Shirikisho, kiungo wake, Said Hamis Ndemla amekuwa kivutio kwa mashabiki wa soka waliokuwa eneo hilo.

Ndemla alionekana kuchangamkiwa na mashabiki wengi wakimuita jina lake na baada ya hapo wakaanza kujadili suala la yeye kuwa na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti wakati ana umbo dogo.

"Anaonekana ni mdogo, lakini mikwaju yake hatari sana yule mtu aisee," alisema mmoja wa mashabiki na kuungwa mkono na wenzake.

Ndemla amekuwa na sifa ya kupiga mashuti makali kiasi cha kujijengea imani hata ya kupata namba katika kikosi chini ya Mfaransa, Pierre Lechantre.


Simba inakwenda Djibouti kucheza mechi yake ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Gendamarie.

Katika mechi ya kwanza, Simba ilishinda kwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic