February 26, 2018


Na George Mganga

Mzunguko wa nne wa mashindano ya Kombe la Shirikisho unatarajia kukamilika leo February 26 2018 kwa mechi mbili kuchezwa.

Katika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga, Stand United itakuwa mwenyeji dhidi ya timu kutoka makao makuu ya nchi, Dodoma FC, mechi ambayo itachezwa saa 10:00 jioni.

Mechi nyingine itakayochezwa ni Kiluvya United ambao wataikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mabatini. Mechi hii itaanza saa 8:00 mchana.

Timu zitakazoshinda leo, zitaingia kwenye hatua ya nane bora, tayari kwa kusubiri droo ya kupangiwa kila timu icheze na nani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic