February 26, 2018



Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka 'SMG', anatarajia kuzichapa na bondia kutoka nchini Thailand ambaye bado hajajulikana ni nani, lakini ameanza mazoezi makali huku akisema kwamba anatumia konokono kama chakula chake ili aweze kumtoa nishai mpinzani wake huyo.

Cheka ambaye kwa sasa ni balozi wa Chama cha Urafiki wa Tanzania na Msumbiji 'Tamofa', amejichimbia mkoani Mtwara akiendelea na maandalizi ya pambano hilo ambalo litakuwa la ubingwa linalotarajiwa kufanyika Aprili Mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nagwanda Sijaona, Mtwara.

Cheka alisema kuwa ameamua kuandaa pambano hilo kwa lengo la kuinua ngumi za kulipwa katika mikoa ya Kusini kwa kuwa ndiyo sehemu alipotokea, hivyo lazima afanye maandalizi makali ili aweze kufikia malengo.

"Nashukuru Mungu huku kila kitu kinaenda sawa na kwa sasa nipo kwenye maandalizi makali kwa ajili ya kucheza na bondia kutoka Thailand.

"Nakula konokono kwa ajili ya kuongeza nguvu ili kazi yangu iwe nyepesi siku hiyo licha ya kuwa mpinzani wangu bado anatafutwa mwenye uwezo na lazima atoke kwenye nchi hiyo.


"Hawa wadadu supu yake ni nzuri asikwambie mtu na ndiyo maana wamekuwa wakisafirishwa kwenda China kwa ajili hiyo, hadi panya mimi nakula, lakini hao konokono kwa sababu ya kuniongezea vitu, kwa sababu watu kutoka Bara la Asia wengi wanatumia kwa kuongeza nguvu," alisema Cheka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic