February 16, 2018


Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, ameibuka na kusema kuwa Benchi la Ufundi la timu ya Yanga likiongozwa na Kocha Mkuu, Mzambia, George Lwandamina, lilichelewa kufanya maamuzi ya mchezaji wa kupiga penalti na kuongeza kuwa, kiungo Papy Tshishimbi atawakomesha wengi kutokana na kufanya kile ambacho alikiona awali.

Awali Mzee Akilimali alitaka benchi hilo la ufundi kuhakikisha wanatafuta mbadala wa mchezaji wa kupiga penalti badala ya Mzambia, Obrey Chirwa ambaye amekuwa hana bahati nazo tofauti na ilivyokuwa awali.

Ikumbukwe kuwa, kwa mwaka huu Chirwa alikosa penalti ya kwanza kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya URA ya Uganda na katika mchezo wa Kombe la  FA dhidi ya Ihefu. Penalti nyingine alikosa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St. Louis ya Shelisheli.

Juzi Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Yanga  ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji ambapo Tshishimbi alifunga mabao mawili moja likiwa ni la penalti.

Mzee Akilimali alisema amepongeza hatua ya benchi la ufundi kumbadilisha Chirwa katika kazi ya kupiga penalti kwa kumpa Tshishimbi ambaye anaamini lazima atakuwa anawakomesha makipa kwani anaitambua vyema kazi iliyomleta kwenye timu hiyo.

“Nadhani kila mtu ameona yule kijana Tshishimbi kwa jinsi alivyopiga penalti safi kabisa tena huwa ananikosha sana kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza mpira tena anatambua kazi yake vilivyo ndani ya Yanga.


“Naamini atakuwa anawakomesha wapinzani, aendelee kupewa jukumu hilo ili tuangalie na kile ambacho tunatakiwa kukifanya,” alisema Mzee Akilimali. 

1 COMMENTS:

  1. Chirwa hana bahati na Mzee Akilimali tokea Chirwa aje nchini. Lakini pia hata Tshishimbi anweza akakosa penati. Haya ngoja tusubiri tuone.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic