February 27, 2018



Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Romelu Lukaku, amesema kuwa anastahili kupewa heshima ndani ya Man United kutokana na kiwango alichonacho katika timu hiyo kwa sasa.

Lukaku aliisadia Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 wikiendi iliyopita, amesema licha ya umri wa wake wa miaka 24 aliyonayo hivi sasa, bado ana uwezo wa kuipambania klabu yake.

Mbali na hayo Lukaku amesema anahitaji pia kushinda mataji mengi na kikosi hicho cha United kwani ana matumaini hayo.

Mpaka sasa mshambuliaji huyo amefikisha jumla ya mabao 27 akiwa United huku akiwa amefunga jumla ya mabao 43 katika msimu huu kwa klabu na taifa lake la Ubelgiji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic