February 27, 2018


Na George Mganga

Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga, Hans van der Pluijm, ametajwa kuwa alikuwa akiingiwa na hofu kubwa na wachezaji Kipre Tcheche aliyechezea Azam FC na Emmanuel Okwi wa Simba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Afisa Habari wa zamani wa Yanga, Jerry Muro, amesema Hans alikuwa anakuwa na wasiwasi pale Okwi anapokuwepo kikosini pindi Simba ikicheza dhidi ya Yanga.

Muro aliligusia hilo wakati akizungumzia namna kiwango cha Okwi kilivyo msimu huu kuelekea kuwania kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

"Hakuna wakati mgumu aliokuwa anakutana nao Kocha Hans kama uwepo wa Okwi na Tchetche upande wa wapinzani wetu, kwa hiyo katika msimu huu Okwi yuko vizuri kuliko Chirwa' alisema Muro wakati akimzunguzia Emmanuel Okwi.

Pluijm ambaye yuko Singida United hivi sasa, aliwahi ifundisha Yanga ambayo inanolewa na Kocha George Lwandamina kutoka Zambia.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic