February 18, 2018





Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa anaamini kikosi chake kitashinda mabao mengi ugenini nchini Shelisheli.

Tayari Yanga iko Shelisheli ikisubiri kuwavaa St Louis katika mechi ya pili baada ya ile ya kwanza kupata ushindi wa bao 1-0.

Nsajigwa amesema: “Walivyocheza hapa itakuwa tofauti na kwao, lazima watafunguka na kutushambulia.

“Kuna mengi yatabadilika, basi tuna uwezo wa kubadilika. Kikubwa sisi tunataka kusonga mbele.”


Yanga imeondoka nchini ikiwa inajiamini kuwa itafanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo ingawa baadhi ya mashabiki wanaonekana kuwa na hofu.

1 COMMENTS:

  1. Hivi hofu inatokea wapi toka lini seychelles imeitoa timu ya Tanzania? Hawa ndio wa kuitoa Yanga? Tufikirie hatua inayofuata ndio tutaanza mechi za ushindani. Seychelles na Djibouti hizi tunazitoa nje.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic