February 18, 2018




Nahodha wa Azam FC, Himid Mao amegundulika na uvimbe katika goti lake na atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu akipata matibabu.

Hali hiyo imegundulika baada ya klabu yake ya Azam FC kumpeleka Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema Himid atakaa nje kwa wiki tatu lakini hatafanyiwa upasuaji.

“Tayari wamempa tiba mbadala, anaanza matibabu huko Afrika Kusini na baadaye anarejea nyumbani na ataendelea na matibabu.

“Maumivu makali ndani ya goti yalikuwa yanatokana na uvimbe uliotengenezwa kutokana na damu kuvilia,” Iddi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic