Na George Mganga
Kuelekea mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Ndanda, Mussa Mbaya, amewatambia Yanga kuwa kesho ni lazima waache alama 3 mkoani Mtwara.
Mbaya amesema anatambua kuwa Yanga wanafukuzana na Simba kuwania ubingwa wa Ligi, lakini wanachokiangalia wao ni ushindi pekee kwenye mchezo huo.
"Sisi tumejiandaa vema, na nawaambia mashabiki wetu wajiandae kupokea alama tatu muhimu, ushindi utakuwa kwetu bila shaka yoyote" amesema Mbaya.
Ndanda itakuwa mwenyeji wa pambano hilo ikicheza mchezo wa 19 sawa na Yanga, lakini utofauti upo katika msimamo ambapo Ndanda ina alama 18, nafasi ya 13 na Yanga 37, nafasi ya pili.
Haya maneno maneno ndo yameiponza timu ya Mbao FC jana, msiwachukulie Yanga poa maana bado wanakikosi kizuri na wachezaji wake wanajituma sana uwanjani. Ndanda chonde chonde jamani yasije wakuta ya jana kwa Mbao tena nyumbani kwenu.
ReplyDeleteWaambie ukweli hao Ndanda kwanza waelewe Yanga sio saizi yao kabisa ni wakubwa wao. Wawaheshimu wacheze mpira kwa tahadhari zote kwa lengo la kuwafunga na hilo litawapa sifa lakini sio kutoa maneno ya kebehi wawaulize wenzao Mbao kilichowapata kwa Simba pale uwanja wa taifa jana. Kilichowaponza maneno yao ya Mwenyekiti wao.
ReplyDeleteNdanda wanahitaji point tatu muhimu kuepukana kushuka daraja. Na hakuna sehemu ya kujaribu kuvuna point tatu 3 muhimu kama si kwenye uwanja wa nyumbani. Wakati mwengine mpira hauna timu kubwa Ndanda wakishindwa kubakiza point tatu kwenye uwanja wao wa nyumbani itabidi wajilaumu wenyewe.
ReplyDelete