February 28, 2018



Beki wa Simba, Asante Kwasi amewafanyia kitu mbaya timu ya Mbao FC ya jijini Mwanza katika mchezo wa juzi uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar, kufuatia kitendo cha kusikiliza maelekezo ya wachezaji waliyokuwa wakipewa na kocha wao ili kujua kinachoendelea ambapo alisema kuwa kitendo hicho ni moja ya mbinu ya kiuanamichezo kuweza kuwamaliza wapinzani wao.

Mara kadhaa Kwasi amekuwa akienda kwenye benchi la wapinzani wake pindi kunapotokea mpira umesimama, wakati wachezaji wanapokwenda kwa kocha kufuata maelekezo mwanzo mwisho.

 

Katika mchezo uliochezwa Jumatatu dhidi ya Mbao, Kwasi alikwenda katika benchi la Mbao zaidi ya mara tatu kusikiliza maagizo waliyopewa wachezaji kisha kwenda kuwaambia wenzie kinachojiri.

Kwasi alisema kuwa, kitendo alichokuwa akikifanya ni mbinu ya kiuanamichezo kuweza kuwamaliza wapinzani wao kwa lengo la kufahamu maelekezo wanayopewa ili kuyafanyia kazi.

“Tumefurahi matokeo haya ya ushindi wa mabao matano, lengo letu ni kuona tunafanikiwa kufanya vizuri kila mechi tunayocheza ili kufanikiwa kutwaa ubingwa mwishoni mwa msimu.

“Mara nyingi nimekuwa nikienda kwa benchi la wapinzani kusikiliza, hii ni moja ya mbinu ya kimchezo  ambayo inasaidia kuwasoma wapinzani wetu na kujua wanataka kufanya nini ili kuweza kujihami, ni mbinu ya kawaida ambayo inafanywa sehemu yoyote,” alisema Kwasi.


 Aidha beki huyo, ana mabao sita hadi sasa aliyoyafunga kwenye ligi huku akiwa amefunga akiwa Lipuli FC matano na moja akiwa  na Simba.

2 COMMENTS:

  1. Asante sana Kwasi... waliokuwa wanahoji usajili wa bil 1.3 ..Sasa hv wanalia na ratiba tu

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli kuhoji kwao imekula kwao, maana kazi wanaonyeshwa kwa kweli. Na ikiwa mechi tatu Simba ikashinda, nafikiri wataendelea kujiuliza tu..... Simba mbele kwa mbele

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic