Ligi ya Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite hatua ya nane bora inaendelea leo Jumatano kwa kupigwa michezo mitatu katika viwanja vitatu tofauti.
Ligi hiyo ilizinduliwa wikiendi iliyopita Mkoani Kigoma kwa kushuhudia Kigoma Queens ikiichapa Simba Queens mabao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika.
Ligi hiyo inayodhaminiwa na kinywaji cha Serengeti Lite, imegawanywa katika makundi mawili, leo Ever Green wataivaa JKT Queens katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar ukiwa ni wa Kundi A.
Michezo mingine miwili itakuwa ni kutoka Kundi B, ambapo Baobab wataikaribisha Panama katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, huku Alliance Queens wakiwa wenyeji wa Kigoma Siterz pale Nyamagana, Mwanza.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi kuchezwa mechi nne ambapo Simba itacheza dhidi ya Ever Green wakati Mlandizi Queen watacheza na Kigoma Sisterz na Baobab dhidi ya Alliance Queens huku Panama wakitarajia kupepetana na JKT Queens.
0 COMMENTS:
Post a Comment